MUHTASARI
WA KIKAO CHA KWANZA CHA KUANZISHA MFUKO
WA KUSAIDIANA KILICHOFANYIKA SIKU YA IJUMAA
TAREHE 05/7/2013 KWENYE PUB YA A-TOWNERS - ARUSHA
1.0
MAHUDHURIO
A: WALIOHUDHURIA
S/
|
JINA
|
WADHIFA
|
1.
|
BARAKA NAHUM
|
MJUMBE
|
2.
|
WILBERT KOMBE
|
MJUMBE
|
3.
|
SHABANI MBIRIZE
|
MJUMBE
|
4.
|
GODFREY NAIMAN
|
MJUMBE
|
5.
|
DEO MATEMU
|
MJUMBE
|
6.
|
DAVID BUHATWA
|
MJUMBE
|
7
|
FRANK NDOSSI
|
MJUMBE
|
8
|
ROBERT NYANGA
|
MJUMBE
|
9
|
PHILIP KOIMERE
|
MJUMBE
|
10
|
FELIX MSHANA
|
MJUMBE
|
B: WASIOHUDHURIA
-
S/
|
JINA
|
WADHIFA
|
1
|
JOSEPH LEWA
|
MJUMBE
|
2
|
LAURIAN SILAYO
|
MJUMBE
|
3
|
CECILIA NDOSSI
|
MJUMBE
|
4
|
MAGRETH NDOSSI
|
MJUMBE
|
5
|
CAMILLA SILAYO
|
MJUMBE
|
6
|
ADAM NNKO
|
MJUMBE
|
7
|
KULT MAJENDO
|
MJUMBE
|
8
|
WALTER MZIRAY
|
MJUMBE
|
9
|
GRACE LYIMO
|
MJUMBE
|
10
|
ANDREW LEBABU
|
MJUMBE
|
2.0
UFUNGUZI WA KIKAO
Mjumbe
aliyeitisha kikao Baraka Nahum aliwashukuru wajumbe wote kwa mahudhurio yao
kwenye kikao hicho na alitangaza
kukifungua rasmi kikao cha kwanza.
3.0
AGENDA
KULIKUWA NA AGENDA
TATU ZA KUJADILIWA KATIKA KIKAO HICHO
1.
Kujadili juu ya kuanzishwa kwa mfuko
wa kusaidiana
2.
Kujadili jina la kikundi
3.
Kuteua kamati ya muda ya kuandaa
rasimu ya katiba ya kikundi
4.
Mengineyo
3.1 AGENDA
NAMBA 1
Kujadili juu ya kuanzishwa kwa kikundi cha
kusaidianana na kutungwa kwa katiba:
Wajumbe tulikubaliana juu ya kuanzisha mfuko wa kusaidiana wakati wa
majanga yanapotokea miongoni mwa jamii zetu. Kutokana na mazingira yetu ya
kazi, kwani muda mwingi tunautumia kazini na kushindwa kushirikiana na jamii
iliyotuzunguka huko mitaani tunapoishi tumejikuta tunakuwa katika wakati mgumu
wa kuyakabili majanga hayo, ambayo aidha hutokea kwa uasilia wake au kwa bahati
mbaya.
Pia
tumeangalia hali ngumu ya maisha inayo zikabili jamii nyingi hapa Arusha na
Nchini kwa ujumla na kwamba Jamii
nyingi kukosa mitaji ya kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa kujiongezea kipato
na kukidhi baadhi ya mahitaji muhimu ya kibanadamu.
Pia
tulijadili juu ya kutungwa kwa katiba ya kikundi ambayo itazingatia mambo
yafuatayo:
·
Mwanachama
kuacha kazi/kujitoa
·
Mwanachama
akiuguliwa atasaidiwaje (atapewa fedha kiasi gani)
·
Mwanachama
akifunga ndoa atasaidiwaje na kikundi
·
Mwanachama
akifiwa na watu wake wa karibu au msiba kuwepo nyumba anayoishi.
·
Kufungua
Account ya kikundi
·
Mahudhurio ya
kikao, wanachama wajitahidi kuhudhuria, hakuta kuwa na lawama kwa wasio
hudhururia kwa lolote litakaloamuliwa na kikao au wanachama waliokuwepo.
·
Kuwezeshana kimtaji
ianze haraka iwezekanavyo kwa lengo la kukuza kikundi hasa upande wa riba.
·
Kuanzia siku ya
leo mwanachama yoyote atakaye patwa na tatizo kubwa wanachana wanawajibu wa
kuwajibika kama kikundi kumsaidia ikiwa ndio dhana kubwa ya kuanzishwa kwa
kikundi hichi.
·
Ikitokea
mwanachama amepatwa na tatizo kubwa kabla ya mfuko kutuna wanachama watatakiwa
kuchanga kutoka kwenye mifuko yao kwaajili ya kumsaidia mwanachama mwenzao.
·
Fain itatolewa
kwa watakao kuwa wanachelewa kwenye kikao au kutohudhuria mara kwa mara kwenye
vikao pasipo sababu maalum.
·
Maendeleo
yanayolengwa kwa ajili ya baadae yawekwe kabisa katika katiba ili kuondoa
usumbufu hapo baadae, kama ujasiliamali n.k.
·
Kwa kuanza
ifunguliwa Account kwakuwa pesa haziwezi
kuwa zinakaa mfukoni kwa mtu ni” risk”.
·
Baada ya
kukamilika kwa katiba kila mwanachama atahitajika kuwa na katiba na aisome na
kuielewa ili tuwe kwenye mstari mmoja.
·
Kuwepo na
kamati ndogo ndogo ndani ya kikundi K.M kamati ya misiba,harusi n.k.
·
Kamati hizo
ndizo zitaleta taarifa ya matumizi ya pesa na yatakayojiri sehemu husika.
·
Kiingilio kwa
wanachama ishirini wa mwanzo ni sh 50000/= na mchango wa kila mwezi ni 20000/=, michango inatakiwa
kuanza kutolewa July, na kiingilio kinatakiwa kuwa kimekamilika mwishoni mwa
mwezi wa tisa
3.2 AGENDA
NAMBA 2
Kujadili jina la kikundi:
Wajumbe walikubaliana kila mmoja apendekeze jina la
kikundi ambapo wajumbe waliomba wapewe muda wa kutafakari, hata hivyo mjumbe
mmoja Baraka Nahum Alipendekeza jina la kikundi liwe ni CYCLE FRIENDS.
Wajumbe wote waliridhia jina hili lipitishwe kwa muda
lakini kama kutakuwa na pendekezo la jina lingine, basi liwasilishwe kwenye
mkutano wa pili wa kikundi kwa ajili ya kupigiwa kura.
3.3 AGENDA
NAMBA 3
Kuteua kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya
kikundi:
Wajumbe
walipendekeza majina ya wajumbe watatu kuingia kwenye kamati ya muda ya kuandaa
rasimu ya katiba ya kikundi na kuiwasilisha kwenye mkutano mkuu wa pili wa kikundi
ambapo kamati hiyo ilipwea mwezi mmoja kukamilisha rasimu hiyo ya katiba.
Wajumbe hao waliochaguliwa na nafasi zao ni hawa
wafuatao:
Jina la mjumbe
|
Wadhifa
|
Shaban
Mbirize
|
Mwenyekiti
|
Baraka
Nahum
|
Katibu
|
Wilbert
Kombe
|
Afisa
Mawasiliano
|
Mwenyekiti
wa muda aliyeteuliwa akizungumza na wajumbe wa kikao hicho aliwashukuru kwa
kumuamini na kumteua kuongoza jahazi hilo la kuanza rasimu ya kikundi. Pia kwa
niaba ya wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo, mwenyekiti alieleza hatua za
awali za kuchukua katika utekelezaji wa kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Mwenyekiti
alitaka wajumbe waanze kutoa michango yao ili pamoja na mambo mengine
ituwezeshe kufanikisha uandaaji wa rasimu hiyo ya katiba. Wajumbe walikubaliana
na wazo hilo na mwenyekiti aliwaomba watoe mapendekezo yao.
Mjumbe
mmoja Deo Matemu alitoa maoni kwamba kila mwanachama atoe kiingilio cha
shilingi 50,000 halafu michango kwa mwezi iwe ni shilingi 20,000 kila mwezi.
Wajumbe
waliafiki, lakini waliomba kiasi hicho cha shilingi 50,000 kisitolewe kwa
mkupuo kwa sababu ya hali ngumu walizo nazo wajumbe waanzilishi. Ilikubaliwa
kishi hicho kilipwe kwa awamu tatu ikiwa ni sambamba na mchango wa kila mwezi wa silingi 20,000.
Hivyo basi iloiamuliwa mwisho mwezi wa Julai kila mwanachama atoe kiasi cha shilingi
20, 000 pamoja na ada ya kiingilio,
Wajumbe
wpte waliafiki wazo hilo na kulipitisha.
3.4 AGENDA
NAMBA 4.
Mengineyo:
Hapakuwa na
hoja zaidi na kila mjumbe aliridhishwa makubalianao hayo.
4.0 KUFUNGA KIKAO
Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe
wote kwa michango yao ya mawazo katika kikao hicho.
Aliwakumbusha wajumbe kuweka
vyema kumbukumbu za kikao hicho ili kuepusha kusahau maazimio waliyoyafanya
wakati wa kikao hicho.
Kikao kijacho kitakuwa tarehe 12/07/2013.
Alitamka kukifunga rasmi kikao
cha 1 cha kikundi cha CYCLE FRIENDS