KIKAO CHA PILI
CHA CYCLE FRIENDS (CF) KILICHOFANYIKA A - TOWNERS TAREHE 12/07/2013
Kikao
kilifunguliwa saa kumi na mbili na nusu jioni.
AGENDA
1. Kufungua kikao
2. Kusoma minutes
za kikao kilichopita
3. Kujadili
uendeshaji wa chama
4. Kujadili michango
ya wanachama na utunzaji wa fedha
5. Mengineyo na
kufunga kikao
1. WALIOHUDHURIA
1. Baraka Kimaro
2. Deogratius
Matemu
3. Wilbert Kombe
4. Godfrey Naiman
5. Robert Nyanga
6. Frank Ndossi
7. Felix Mshana
8. Josephat Kimani
9. Maggie Ndossi
2. WALIOTOA TAARIFA
·
Joseph
Lewa
3.
KUSOMA MINUTES ZA KIKAO KILICHOPITA
3.1 Kamati zilizokuwa zimepewa kazi za kufanya zilitoa ripoti kama ifuatavyo:-
3.1.1 Kamati ya Katiba
3.1 Kamati zilizokuwa zimepewa kazi za kufanya zilitoa ripoti kama ifuatavyo:-
3.1.1 Kamati ya Katiba
Katika
kikao hiki waliopewa jukumu la kushughulikia katiba hawakuweza kuja na majibu
husika kutokana na kubanwa na majukumu ya kikazi.
3.2 Kamati ya Fedha, Kufungua akaunti ya chama
3.2 Kamati ya Fedha, Kufungua akaunti ya chama
Mjumbe
katika kamati hii alikuwa ni Wilbert Kombe ambaye alitoa ripoti yake kuhusiana
na kufungua akaunti katika bank ya Equity ambayo masharti na vigezo vyake vina
unafuu kuliko bank zingine. Hakuweza kufungua akaunti maana alikuwa anasubiria kuleta
ripoti kwa wanachama kwanza.
4.
KUJADILI UENDESHAJI WA CHAMA
4.1
AJENDA
4.1.1
AKAUNTI
4.1.2 KATIBA
4.1.3 MICHANGO
4.1.1 Akaunti ya chama
Baada ya kujadili ripoti ya Bw. Wilbert
Kombe ikaonekana kuwa tuhitaji kufungua akaunti haraka iwezekanavyo na kuwa itafunguliwa
Joint Account kabla ya tarehe 26 mwezi wa saba 2013 Equity Bank, wajumbe
walipendekeza kuwa kuwe na signatories wanne na kuwa walipendekezwa Maggie
Ndossi, Camilla Silayo, Godfrey Naiman na Robert Nyanga. Wajumbe walipendekeza
pia kwa wale watakao kuwa wanatoa michango yao kwa njia ya huduma za simu, basi
fedha hizo ziwe zinatumwa kwa Maggie Ndossi
4.1.2
Kamati ya kufuatilia Katiba ya kikundi
Wajumbe walipendekeza kuwa ili kuwa na
miongozo iliyonyooka na kuondoa utata katika kikundi basi itengenezwe Katiba
kwa haraka ambayo itatakiwa kuletwa mbele za wajumbe katika kikao kijacho kwa
ajili ya kusomwa ili kuona kama imekidhi matakwa ya wanakikundi. Wanaohusika kuandaa
Katiba ni Deo Matemu, Baraka Nahum, Frank Ndossi na Wilbert Kombe. Katika kikao
kijacho watuletee nakala ya katiba itakayokuwa tayari na tutaifanyia
marekebisho pale inapobidi, Deo Matemu akaombwa awe mwenyekiti wa kamati hii.
4.1.3
Michango ya wanachama
Wajumbe walikubaliana kwa pamoja kuwa
kila mwanachama anatakiwa kulipa kiingilio cha uanachama kwa kiwango cha
Shilingi elfu hamsini, ambao kiwango hicho kitalipwa kwa mkupuo ama kwa awamu
katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi wa saba. Vile vile kila
mwanachama anapaswa kulipa ada ya uanachama ya shilingi elfu ishirini kila
mwezi na mwanachama ahakikishe amelipa kiwango hicho kila mwisho wa mwezi bila
kushurutishwa.
Kikao kilifungwa kwa kusisitiza kuwa akaunti
namba itumwe kwa wanachama kabla ya tarehe 26th July 2013, Na pia tukikoseana
tujifunze kusamehe na kusahau yaliyopita wote tuanze ukurasa mpya.
Kikao kingine kitakuwa Ijumaa tarehe 26/07/2012
saa kumi na mbili kamili jioni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni