Alhamisi, 10 Oktoba 2013

MUHTASARI WA KIKAO CHA KWANZA CHA KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIANA KILICHOFANYIKA SIKU YA IJUMAA TAREHE 05/7/2013 KWENYE PUB YA A-TOWNERS - ARUSHA



MUHTASARI WA KIKAO CHA  KWANZA CHA KUANZISHA MFUKO WA KUSAIDIANA KILICHOFANYIKA SIKU YA IJUMAA  TAREHE 05/7/2013 KWENYE PUB YA A-TOWNERS - ARUSHA

1.0       MAHUDHURIO
          A:       WALIOHUDHURIA
S/
JINA
WADHIFA
1.
BARAKA NAHUM
MJUMBE
2.
WILBERT KOMBE
MJUMBE
3.
SHABANI MBIRIZE
MJUMBE
4.
GODFREY NAIMAN
MJUMBE
5.
DEO MATEMU
MJUMBE
6.
DAVID BUHATWA
MJUMBE
7
FRANK NDOSSI
MJUMBE
8
ROBERT NYANGA
MJUMBE
9
PHILIP KOIMERE
MJUMBE
10
FELIX MSHANA
MJUMBE


B:  WASIOHUDHURIA  - 

S/
JINA
WADHIFA
1
JOSEPH LEWA
MJUMBE
2
LAURIAN SILAYO
MJUMBE
3
CECILIA NDOSSI
MJUMBE
4
MAGRETH NDOSSI
MJUMBE
5
CAMILLA SILAYO
MJUMBE
6
ADAM NNKO
MJUMBE
7
KULT MAJENDO
MJUMBE
8
WALTER MZIRAY
MJUMBE
9
GRACE LYIMO
MJUMBE
10
ANDREW LEBABU
MJUMBE



2.0       UFUNGUZI WA KIKAO
Mjumbe aliyeitisha kikao Baraka Nahum aliwashukuru wajumbe wote kwa mahudhurio yao kwenye  kikao hicho na alitangaza kukifungua rasmi kikao cha kwanza.

3.0       AGENDA

KULIKUWA NA AGENDA TATU ZA KUJADILIWA KATIKA KIKAO HICHO
1.   Kujadili juu ya kuanzishwa kwa mfuko wa kusaidiana
2.   Kujadili jina la kikundi
3.   Kuteua kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi
4.   Mengineyo

3.1  AGENDA NAMBA 1
Kujadili juu ya kuanzishwa kwa kikundi cha kusaidianana na kutungwa kwa katiba:
Wajumbe tulikubaliana juu ya kuanzisha mfuko wa kusaidiana wakati wa majanga yanapotokea miongoni mwa jamii zetu. Kutokana na mazingira yetu ya kazi, kwani muda mwingi tunautumia kazini na kushindwa kushirikiana na jamii iliyotuzunguka huko mitaani tunapoishi tumejikuta tunakuwa katika wakati mgumu wa kuyakabili majanga hayo, ambayo aidha hutokea kwa uasilia wake au kwa bahati mbaya.

Pia tumeangalia hali ngumu ya maisha inayo zikabili jamii nyingi hapa Arusha na Nchini kwa ujumla na kwamba   Jamii nyingi kukosa mitaji ya kuanzisha biashara ndogo ndogo kwa kujiongezea kipato na kukidhi baadhi ya mahitaji muhimu ya kibanadamu.
Pia tulijadili juu ya kutungwa kwa katiba ya kikundi ambayo itazingatia mambo yafuatayo:
·         Mwanachama kuacha kazi/kujitoa
·         Mwanachama akiuguliwa atasaidiwaje (atapewa fedha kiasi gani)
·         Mwanachama akifunga ndoa atasaidiwaje na kikundi
·         Mwanachama akifiwa na watu wake wa karibu au msiba kuwepo nyumba anayoishi.
·         Kufungua Account ya kikundi
·         Mahudhurio ya kikao, wanachama wajitahidi kuhudhuria, hakuta kuwa na lawama kwa wasio hudhururia kwa lolote litakaloamuliwa na kikao au wanachama waliokuwepo.
·         Kuwezeshana kimtaji ianze haraka iwezekanavyo kwa lengo la kukuza kikundi hasa upande wa riba.
·         Kuanzia siku ya leo mwanachama yoyote atakaye patwa na tatizo kubwa wanachana wanawajibu wa kuwajibika kama kikundi kumsaidia ikiwa ndio dhana kubwa ya kuanzishwa kwa kikundi hichi.
·         Ikitokea mwanachama amepatwa na tatizo kubwa kabla ya mfuko kutuna wanachama watatakiwa kuchanga kutoka kwenye mifuko yao kwaajili ya kumsaidia mwanachama mwenzao.
·         Fain itatolewa kwa watakao kuwa wanachelewa kwenye kikao au kutohudhuria mara kwa mara kwenye vikao pasipo sababu maalum.
·         Maendeleo yanayolengwa kwa ajili ya baadae yawekwe kabisa katika katiba ili kuondoa usumbufu hapo baadae, kama ujasiliamali n.k.
·         Kwa kuanza ifunguliwa Account  kwakuwa pesa haziwezi kuwa zinakaa mfukoni kwa mtu ni” risk”.
·         Baada ya kukamilika kwa katiba kila mwanachama atahitajika kuwa na katiba na aisome na kuielewa ili tuwe kwenye mstari mmoja.
·         Kuwepo na kamati ndogo ndogo ndani ya kikundi K.M kamati ya misiba,harusi n.k.
·         Kamati hizo ndizo zitaleta taarifa ya matumizi ya pesa na yatakayojiri sehemu husika.
·         Kiingilio kwa wanachama ishirini wa mwanzo ni sh 50000/= na mchango  wa kila mwezi ni 20000/=, michango inatakiwa kuanza kutolewa July, na kiingilio kinatakiwa kuwa kimekamilika mwishoni mwa mwezi wa tisa




3.2  AGENDA NAMBA 2
Kujadili jina la kikundi:
Wajumbe walikubaliana kila mmoja apendekeze jina la kikundi ambapo wajumbe waliomba wapewe muda wa kutafakari, hata hivyo mjumbe mmoja Baraka Nahum Alipendekeza jina la kikundi liwe ni CYCLE FRIENDS.
Wajumbe wote waliridhia jina hili lipitishwe kwa muda lakini kama kutakuwa na pendekezo la jina lingine, basi liwasilishwe kwenye mkutano wa pili wa kikundi kwa ajili ya kupigiwa kura.

3.3  AGENDA NAMBA 3
Kuteua kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi:
Wajumbe walipendekeza majina ya wajumbe watatu kuingia kwenye kamati ya muda ya kuandaa rasimu ya katiba ya kikundi na kuiwasilisha kwenye mkutano mkuu wa pili wa kikundi ambapo kamati hiyo ilipwea mwezi mmoja kukamilisha rasimu hiyo ya katiba.

Wajumbe hao waliochaguliwa na nafasi zao ni hawa wafuatao:

Jina la mjumbe
Wadhifa
Shaban Mbirize
Mwenyekiti
Baraka Nahum
Katibu
Wilbert Kombe
Afisa Mawasiliano

Mwenyekiti wa muda aliyeteuliwa akizungumza na wajumbe wa kikao hicho aliwashukuru kwa kumuamini na kumteua kuongoza jahazi hilo la kuanza rasimu ya kikundi. Pia kwa niaba ya wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo, mwenyekiti alieleza hatua za awali za kuchukua katika utekelezaji wa kuanzishwa kwa kikundi hicho.
Mwenyekiti alitaka wajumbe waanze kutoa michango yao ili pamoja na mambo mengine ituwezeshe kufanikisha uandaaji wa rasimu hiyo ya katiba. Wajumbe walikubaliana na wazo hilo na mwenyekiti aliwaomba watoe mapendekezo yao.

Mjumbe mmoja Deo Matemu alitoa maoni kwamba kila mwanachama atoe kiingilio cha shilingi 50,000 halafu michango kwa mwezi iwe ni shilingi 20,000 kila mwezi.

Wajumbe waliafiki, lakini waliomba kiasi hicho cha shilingi 50,000 kisitolewe kwa mkupuo kwa sababu ya hali ngumu walizo nazo wajumbe waanzilishi. Ilikubaliwa kishi hicho kilipwe kwa awamu tatu ikiwa ni sambamba  na mchango wa kila mwezi wa silingi 20,000. Hivyo basi iloiamuliwa mwisho mwezi wa Julai kila mwanachama atoe kiasi cha shilingi 20, 000 pamoja na ada ya kiingilio,
Wajumbe wpte waliafiki wazo hilo na kulipitisha.

3.4  AGENDA NAMBA 4.
Mengineyo:
Hapakuwa na hoja zaidi na kila mjumbe aliridhishwa makubalianao hayo.
4.0     KUFUNGA KIKAO
Mwenyekiti aliwashukuru  wajumbe wote kwa michango yao ya mawazo katika kikao hicho.
Aliwakumbusha  wajumbe kuweka vyema kumbukumbu za kikao hicho ili kuepusha kusahau maazimio waliyoyafanya wakati wa kikao hicho.

Kikao kijacho kitakuwa tarehe 12/07/2013.
Alitamka kukifunga  rasmi kikao cha 1 cha kikundi cha CYCLE FRIENDS

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni